NANDY

Sauti ya asali ya mwimbaji Nandy ni moja kati ya wasanii walio juu nchini Tanzania akiwa na albamu yake ya “The African Princess”, iliyotoka mwaka 2018. Anafahamika kwa ngoma kama “One Day”, “Nagusa Gusa”, “Aibu”, “Njiwa” na Willy Paul pamoja na “Ninogeshe”; Mshindi wa tuzo ya 2017 kama Best Female Artist East Africa za AFRIMMA ameitingisha tasnia ya muziki ya Africa Mashariki. Nandy alishirikiana na mwimbaji wa Ethiopia Betty G mwaka 2017 kwenye Coke Studio Africa. Nandy anarudi msimu wa mwaka 2019 na Mnaigeria Skales, huku kolabo yao ikisimamiwa na produza GospelOnDeBeatz (Nigeria).

 

CAREER

Nandy alitimba kwenye tasnia ya muziki mwaka 2010 aliporekodi Nyimbo zake tatu za mwanzo. Baadae alijiunga na bendi ya Tanzania: B Band, akiwa pamoja na Banana Zorro kwa miaka kadhaa. Mtusuo wake kwenye umaarufu ulikuja baada ya kuwa sehemu ya mashindano ya Tecno-Own-the-Stage mwaka 2015/2016. Licha ya kuibuka namba mbili, alipokelewa vizuri ndani na nje ya Tanzania, kwenye shoo hiyo iliyofanyika Nigeria, Nandy aliingia kwenye ustaa. Kufuatia mafaniko yake alijiunga na lebo ya THT MEDIA na kuachia ngoma yake ya “Bye” (My Ex).  

 

MUSIC INTERESTS

Ngoma za Nandy zinafanya vizuri sana kwenye vituo vya redio na TV nchini Tanzania shukrani kwa mashabiki wake. Hata hivyo, “Kivuruge” na “Ninogeshe” zimefikisha watazamaji zaidi ya milioni 6 kwenye YouTube. Nandy ameshirikiana na wakali wa Tanzania kama Aslay kwenye “Subalkheri”, Chege kwenye “Kelele za Chura” na Ice Boy kwenye “Binadamu”. Nandy pia ni mfanyabiashara, na anamiliki kampuni yake mwenyewe ya bidhaa za urembo: Nandy Beauty Products na Nandi African Prints.

 

BACKGROUND

Nandy alizaliwa na kupewa jina Faustina Charles Mfinaga mwaka 1992 na wazazi Maria Charles Mfinaga na Charles Wilfred Mfinaga mjini Moshi, kaskazini mwa Tanzania. Alisoma shule ya msingi Julius Kambarage Nyerere na baadae akajiunga na Lomwe High School. Nandy alisoma CBE College of Business Education jijini Dar es Salaam. Akiwa na miaka 6, Nandy tayari alianza kuimba kanisani , akiwa na miaka 15 alianza kukuza muziki wake.