NADIA MUKAMI

Kwa muda wa miaka mitatu tu tangu aingie kwenye tasnia ya muziki wa Kenya, Nadia Mukami tayari ameshafahamika kama mmoja wa sauti ya kuangaliwa nchini. Mwimbaji huyu ambaye pia ni mwandishi ana ngoma kibao ikiwemo “Si Rahisi”, “African Lover” na “Yule Yule”. Anatokea kwenye Coke Studio Africa 2019 kwenye segment ya Big Break, akiwa na Juma Jux (Tanzania) na Shellsy Baronet (Mozambique), ikisimamiwa na produza Lizer  toka Tanzania.

 

CAREER

Nadia alianza kuingia kwenye tasnia ya muziki mwaka 2015 aliporekodi ngoma yake ya “Barua Ya Siri” akiwa yupo chuo. Wimbo wake uliomtoa wa “Kesi” ulipokelewa na kuchezwa sana na kumpa nafasi ya kupafomu na wakali wa Kenya kwenye majukwaa makubwa kama Blaze by Safaricom (Kisumu), The Nile Festival and The Luo Festival, na mengineyo. Mwaka mmoja baadae aliibuka mshindi wa KTN’s Kipawa Show na alifika fainali kwenye Jenga Talanta show — iliyompa jina kubwa la ustaa wake. Miaka miwili katika tasnia Nadia alisainiwa na lebo ya Hailemind Entertainment, na tangu hapo ameachia ngoma tatu kali chini ya uongozi huo mpya.

 

MUSIC INTERESTS

Staili ya muziki wake inatokana na muziki laini ukiwa na ushairi na afro-pop. Amekuwa mshairi tangu sekondari ndio maana ushairi upo ndani ya muziki wake. Kuanza kwake muziki akiwa na umri wa miaka 17, kumetokana na baba yake aliyekuwa msikilizaji mkubwa wa muziki wa Taarab pamoja na kuvutiwa na msanii kutoka Tanzania, mwimbaji Ray C.

 

BACKGROUND

Alizaliwa Nairobi kwa jina Mukami Mwendo, Nadia amesoma shule ya msingi Kari na baadae shule ya sekondari Mount Laverna. Kisha baadae alijiunga na Maseno University kufanya shahada ya uhasibu. Alirekodi wimbo wake wa kwanza wa “Narudi” unaoelezea hali ya mpenzi aliyepotea. Alipokuwa chuo alisimama kufanya muziki na kujiunga na Equator FM – kituo cha radio cha chuo ambapo alikuwa akitangaza kipindi cha ‘Saturday Hip-hop Count’. Baadae aliacha kutangaza na kuendelea na muziki.