SHEEBAH KARUNGI

Mkali na mnenguaji anayependwa Uganda Sheebah Karungi aliingia kwenye muziki na kundi zima la wanenguaji la Obsessions. Amekuwa kwenye chati tangu alipoanza kufanya kazi kivyake na hata kushinda tuzo kadhaa ikiwemo Female Artist of the Year na Artist of The Year kupitia Uganda Music Awards (2017). Sheebah mkali mwenye ngoma zilizofanya vizuri barani kama “Nkwatako”, “Mummy Yo” na “Binkolera”. Anarudi kwenye Coke Studio Africa mwaka 2019 akishirikiana na Harmonize (Tanzania) na GospelOnDaBeatz (Nigeria).

 

CAREER

Tangu aingie kwenye tasnia mwaka 2006 na Obsessions, Sheebah amekuwa akisonga mbele kivyake. Mwaka 2010 aliachia ngoma yake ya kwanza "Kunyenyenza" ikifuatiwa na "Bulikyekola" akimshirikisha KS Alpha na "Baliwa" akiwa na Coco Finger. Kiufupi ana albamu nne za studio: Ice Cream (2014), Siri Zari (2015), Nkwatako (2016) na Karma Queen (2017).

 

MUSIC INTERESTS

Mafanikio ya muziki wa Sheebah umemfanya ashinde tuzo kadhaa nchini Uganda kama Best Female Artist tangu 2014 hadi leo. Mwaka 2017, alishinda Best Collaboration of The Year kupitia Zzina Awards. Mwaka huo huo, aliwania kipengele cha Best Female Artist Africa kupitia Nigeria Entertainment Awards na Young Achievers Award katika Sanaa ya ubunifu. Video yake ya “Kisasi Kimu” ilipata kuwania tuzo ya Video of The Year kupitia MTV Mama Awards (2016). Mara kwa mara ameshiriki HiPipo Music Awards na Uganda Entertainment Awards. Pia ni mwigizaji, alishiriki filamu ya Disney ya mwaka 2016, Queen of Katwe.

 

BACKGROUND

Sheebah Karungi alizaliwa na kukulia Kawempe nchini Uganda, na baada ya kumaliza elimu yake kwenye shule ya msingi ya Kawempe Muslim, alijiunga na shule ya sekondari ya Midland, akiwa na umri wa miaka 15, alianza kucheza na kujiunga na kundi la kucheza muziki lililoitwa Stingers kabla ya kuondoka kwenye kundi hilo na kujiunga na Obsessions mwaka 2006, Alipokuwa Obsessions ndiko alipozidi kuimarika na kuupenda Zaidi muziki na kufanya rekodi ya nyimbo mbili kabla ya kuamua kuachana na kundi hilo.